Usimamizi wa Biashara na Fedha

Njia Rahisi Kufunga Hesabu Bila Kupoteza Muda na Makosa

Mwongozo rahisi wa mahesabu ya Wakala unakuonyesha hatua kwa hatua namna ya kuhesabu float, cash, madeni na formula zote za kimahesabu.

28 Mei 2026
Sirily Lasway (AgentsLog)

1. Mfumo wa Kufunga Hesabu za kila siku

Kabla ya kuangalia siku moja baada ya nyingine, mfumo unatumia kanuni mbalimbali ambazo ni muhimu kurahishisha hesabu :

  • Mtaji Mkuu (Capital = Mfano tutatumia: Tsh 1,000,000): Hii ndo mtaji wako uliowekeza tutakoutumia kila siku, na ni nadra sana kubadilika
  • Fomula Kuu ya Kufunga Siku: Total=Cash+Float+Expenses+Debit(Receivables)−Credit(Payables)\text{Total} = \text{Cash} + \text{Float} + \text{Expenses} + \text{Debit(Receivables)} - \text{Credit(Payables)}
  • Lengo la Siku ya Kawaida: Salio la mwisho (Balance=Total−Capital\text{Balance} = \text{Total} - \text{Capital}) lazima liwe 0 ina maana hatuna shoti yaani kusiwe na ziada au upungufu.
  • Expenses: Matumizi yote ya biashara
  • Debit (Receivables): Fedha tunazodai, kutokana na kukopesha, kutoa huduma ila bado hatujapokea fedha
  • Credit (Payables): Fedha tunazodaiwa kutokana na mkopo, kupokea pesa ila bado muamala hujafanyika

Awamu ya Kwanza: Mzunguko wa Siku 5 za Mwanzo

Siku ya 1:

Hapa tunafunga siku tukiwa na taarifa zifuatazo:

KipengeleKiasi (Tsh)
Cash300,000
Float620,000
Expenses10,000
Debit20,000
Credit5,000

Hesabu ya Jumla (Total): 300,000+620,000+10,000+20,000−5,000=945,000300,000 + 620,000 + 10,000 + 20,000 - 5,000 = \mathbf{945,000}

Salio la Siku (Balance): 945,000−1,000,000=−55,000945,000 - 1,000,000 = \mathbf{-55,000}

Uamuzi wa Kihesabu: Hesabu imekuwa less, tukagundua tuna upungufu/Short ya Tsh 55,000. Ili kuilinda hesabu isipotee, tunamua kuandika kiasi hiki kama Loss upande wa Credit kuanzia siku inayofuata.


Siku ya 2:

Tunafunga siku ya pili huku tukibeba ile hasara ya jana (55,000) na kuongeza deni lingine la 20,000:

KipengeleKiasi (Tsh)
Cash400,000
Float500,000
Expenses (Umeme)125,000
Debit50,000
Credit (Loss + Deni)75,000

Hesabu ya Jumla (Total): 400,000+500,000+125,000+50,000−75,000=1,000,000400,000 + 500,000 + 125,000 + 50,000 - 75,000 = \mathbf{1,000,000}

Salio la Siku (Balance): 1,000,000−1,000,000=01,000,000 - 1,000,000 = \mathbf{0}

Uamuzi wa Kihesabu: Siku hii haina shoti. Hesabu imebalance vizuri imesoma 0, kumaanisha hakuna upotevu mpya wa pesa uliotokea ndani ya mzunguko wa siku hii.


Siku ya 3:

Siku hii mteja akaturudishia Tsh 25,000 ya deni, hivyo Debit ikapungua. Pia tumelipia internet, na Credit ikabaki kuwa ile hasara ya mwanzo tu hivyo hesabu za jioni zinakuwa:

KipengeleKiasi (Tsh)
Cash425,000
Float440,000
Expenses (Umeme 125k + Wifi 30k)155,000
Debit25,000
Credit55,000

Hesabu ya Jumla (Total): 425,000+440,000+155,000+25,000−55,000=990,000425,000 + 440,000 + 155,000 + 25,000 - 55,000 = \mathbf{990,000}

Salio la Siku (Balance): 990,000−1,000,000=−10,000990,000 - 1,000,000 = \mathbf{-10,000}

Uamuzi wa Kihesabu: Tumepata upungufu wa Tsh 10,000. Hii inarekodiwa kama hasara mpya ya kupelekwa mbele.


Siku ya 4:

Tukamkopesha mtu 15,000 (Deni la leo), tunachukua hasara ya jana (10,000) ukaijumlisha na credits zilizopita (55,000) hesabu ya jioni inakuwa:

KipengeleKiasi (Tsh)
Cash325,000
Float560,000
Expenses155,000
Debit25,000
Credit (55k + 10k + 15k)80,000

Hesabu ya Jumla (Total): 325,000+560,000+155,000+25,000−80,000=985,000325,000 + 560,000 + 155,000 + 25,000 - 80,000 = \mathbf{985,000}

Salio la Siku (Balance): 985,000−1,000,000=−15,000985,000 - 1,000,000 = \mathbf{-15,000}

Uamuzi wa Kihesabu: Tunapata shoti ya Tsh 15,00, hapa kuna upungufu. Hii inarekodiwa kama Loss kwenye Credit


Siku ya 5:

Tunafunga hesabu jioni tukiwa tumerekodi tumelipwa madeni, tukalipia deni la 20,000, na kuongeza matumizi ya chakula (10,000):

KipengeleKiasi (Tsh)
Cash350,000
Float555,000
Expenses (155k + 10k)165,000
Debit45,000
Credit (80k + 15k - 20k)75,000

Hesabu ya Jumla (Total): 350,000+555,000+165,000+45,000−75,000=1,040,000350,000 + 555,000 + 165,000 + 45,000 - 75,000 = \mathbf{1,040,000}

Salio la Siku (Balance): 1,040,000−1,000,000=+40,0001,040,000 - 1,000,000 = \mathbf{+40,000}

Uamuzi wa Kihesabu: Kuna ziada/shoti ya ziada ya Tsh +40,000. Hii itarekodiwa kama Excess kwenye Debit


Awamu ya Pili: Kuingia Mwezi Mpya (Kukuza Mtaji)

Mwanzoni mwa mwezi tumepata Commission ya Tsh 725,000, na tulikuwa na mlundikano wa Expenses za Tsh 300,000. Hapa ndipo tunapotumia njia ya kulipa matumizi yetu ya kibiashara:

Hatua ya Kulipia Gharama (Pay Up Expenses)

Hapa tuna kata gharama za matumizi ya mwezi ulipoita moja kwa moja kutoka kwenye kamisheni tuliyolipwa:

Kamisheni Safi iliyobaki (Net Commission): 725,000−300,000=425,000725,000 - 300,000 = \mathbf{425,000}

Gharama (Expenses) zikawa 0 (Paid up) kwa sababu zimeshatatuliwa.

Hesabu ya Mwezi Mpya (Day 1) — Mtaji ukiwa bado Constant (1,000,000)

Tumefungua daftari la mwezi mpya tukiwa na taarifa hizi katika mojawapo ya siku:

KipengeleKiasi (Tsh)
Cash400,000
Float1,250,000
Debit50,000
Credit35,000
Expenses0 (Umeshaifuta kwa kamisheni)
Net Commission425,000

Fomula: Total=Cash+Float+Debit+Expenses−Net Commission−Credit\text{Total} = \text{Cash} + \text{Float} + \text{Debit} + \text{Expenses} - \text{Net Commission} - \text{Credit}

Hesabu ya Jumla (Total): 400,000+1,250,000+50,000−425,000−35,000=1,240,000400,000 + 1,250,000 + 50,000 - 425,000 - 35,000 = \mathbf{1,240,000}

Salio la Mwisho (Total Balance): 1,240,000−1,000,000=+240,0001,240,000 - 1,000,000 = \mathbf{+240,000}


Hitimisho na Mkakati Tutakochagua

Kwa kufuata kanuni hizi za hesabu ya uwakala: kila siku salio liwe 0 huzuia wizi au upotevu, na pia mtaji uongezeke tu mwanzoni mwa mwezi baada ya kutoa gharama zote ndani ya faida/kamisheni. Hii inarahisha hesabu zako na inakuba uwezo wa kuewza kufuatilia bishahara yako vizuri na kuepuka makosa na kuchanganya hesabu na hasara

Kutokana na hiyo ziada ya Tsh 240,000, sasa hivi unaweza kuongeza kwenye mtaji wako hivyo mtaji wetu mpya utakuwa Tsh 1,240,000 au kuweka kama faida kwa matumizi mengine.